MWANAFUNZI WA CHUO CHA UGUZI KAHAMA,AKUTWA AMEKUFA KWENYE KARAVATI MJINI SHINYANGA.


Mkazi wa Kata ya Mwasele Manispaa ya Shinyanga  HENRY MWALONGO (48) ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi Kahama mkoani Shinyanga amekutwa akiwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa umeharibika ndani ya kalavati mjini Shinyanga. 

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SIMON HAULE, mwili wa HENRY ambaye ni mkazi wa kata ya Mwasele katika Manispaa ya Shinyanga ulikutwa katika kalavati hilo Aprili 6  mwaka huu katika eneo la Kambarage mjini Shinyanga. 

Kamanda Haule ameleeza kuwa inakadiriwa kuwa mwili huo ulikuwa ndani ya kalavati hilo kwa muda wa siku tano na sehemu kubwa ya mwili wake ilikuwa imezama kwenye mchanga. 

Amesema baadhi ya ndugu wa marehemu wameeleza kuwa marehemu alikuwa na tabia za kunywa pombe kupindukia na hilo lilikuja kujithibitisha baada ya kumkuta akiwa na chupa ya pombe kali katika mfuko wa koti lake alilokuwa amevaa.

Amefafanua kuwa chanzo cha kifo hicho bado kinachunguzwa kwani kifo chake kinatia mashaka. 

Katika Tukio jingine,  AHMED ALLY AMIRI amefariki dunia baada ya gari aliyokuwa anaendesha kuacha njia na kutumbukia mtaroni katika eneo la Ushirika barabara ya Shinyanga kuelekea Mwanza. 

Kamanda HAULE amesema ajali hiyo imetokea jana Aprili 7 majira ya saa tisa alfajiri wakati gari lenye namba za usajili T.529 BHC Toyota Land Cruiser akiendesha alilokuwa Marehemu AMIRI kutokea Shinyanga kuelekea Maganzo kuacha njia na kutumbukia mtaroni na kusababisha kifo chake papo hapo. 

Kamanda HAULE amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi hivyo kusababisha kushindwa kumudu kukata kona na hivyo kuingia mtaroni.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata