MKAZI WA NYAHANGA KAHAMA ANUSURIKA KUUWAWA AKITUHUMIWA KUIBA NUSU KILO YA NYAMA BUCHANI.

MUUZA NYAMA KATIKA BUCHA AMBALO MTUHUMIWA HUYO AMEIBA NYAMA BWANA JOSEPH JOHN.
KAHAMA

Mkazi wa Nyahanga  mjini Kahama  RAMADHAN HAMIS (36) amenusurika kuuawa na wananachi  wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuiba nyama  katika bucha Moja iliyopo Mtaa wa Nyahanga.

Tukio hilo  hilo limetokea leo  majira ya saa tatu asubuhi ambapo RAMADHAN anadaiwa kufika katika bucha hiyo na kuomba apimiwe nusu kilo ya Nyama yenye thamani ya Shilingi  3000.

Akizungumza na Kijukuu Blog, Muuzaji wa bucha Hiyo  JOHN JOSEPH amesema  Mtuhumiwa  huyo alifika katika  bucha hiyo na kumwambia kuwa ampimie kiasi hicho cha nyama ili ampeleke kwenye hoteli ya mke wake iliyopo jirani na bucha hiyo ambapo pia aliomba pesa aifuate hapo.

Alisema baada ya kumpimia Nyama  mtuhumiwa (RAMADHAN) alikwenda kwenye hoteli hiyo na kisha kutoka  pasipo kulipa ambapo alimuomba alipe pesa hiyo kama alivyoahidi ambapo alianza kukimbia na ndipo wananchi walipoanza kumfukuza na kisha kumkamata.

Naye RAMADHAN ambaye ni Mtuhumiwa amesema  amekuwa akienda kukopa kwenye  bucha  kutokana na  muuzaji wa zamani  aliyemuita MURA,  hivyo ni kama mazoea kwake kwenda pale kukopa na kulipa baadaye.

Mmoja wa Mashuhuda  ERIC JOHN ambaye anaegesha  pikipiki eneo hilo, amesema hajawahi kumuona katika eneo hilo mtuhumiwa huyo    na kwamba alifika asubuhi akanunua  pombe  ya shilingi 1000, katika duka moja lililopo eneo hilo ambapo baada ya kudaiwa pesa aliamua kuacha simu yake kama mdhamana.

Hata  hiyo  wanawake wanauza  hoteli katika eneo hilo  wamesema hawamjui mtuhumiwa huyo na kwamba alifika hapo kisha kuondoka huku akiwaambia kuwa  ni fundi ujenzi ambapo kunavijana wake watakuja kunywa chai baadaye.


Hata hivyo  msamaria Mmoja alimlipia kiasi hicho cha fedha kwenye bucha hiyo pamoja na kwenye duka analodaiwa kisha wananchi wakamuachia akaenda zake.

MATUKIO KATIKA PICHA:
 MTUHUMIWA WA WIZI WA NYAMA RAMADHANI HAMISI AKIWA ANAONDOKA ENEO LA TUKIO MARA BAADA YA MSAMALIA MWEMA KUMLIPIA DENI LA NYAMA

 MTUHUMIWA WA WIZI WA NYAMA AKIKUBALI KUTENDA KOSA HILO NA KUSEMA KUWA TATIZO NI MAZOEA.

 MTUHUMIWA AKITOA MAELEZO KWA MWANDISHI WA KIJUKUU BLOG ALIYEKUWEPO ENEO LA TUKIO.

 HUYU NDIYE MTUHUMIWA WA WIZI WA NYAMA NUSU KILO ALIYENUSULIKA KICHAPO LEO MJINI KAHAMA
HII NDIYO HOTEL AMBAPO MTUHUMIWA ALISEMA KUNA MKE WAKE NA NDIPO ALIPOPELEKA NYAMA LAKINI MAMA HUYO ALIKANA KUMTAMBUA 
SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata