MCHINA ‘ALIYETELEKEZA’ MTOTO DAR ATAFUTWA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema baba wa mtoto wa Kichina aliyesambazwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya mama yake kufika ofisini kwake akidai kutelekezwa, anatafutwa.

Makonda ameyasema hayo leo Aprili 14 katika mahojiano maalumu yanayorushwa na televisheni ya TBC.

Amesema: “Kuhusu yule mtoto wa kichina nimefanya mawasiliano na ubalozi wa China, tumewatumia ‘details’ ili yule baba aweze kutafutwa.”

Makonda amesema kama baba wa mtoto huyo asipopatikana, Taifa litakuwa na wajibu wa kumtunza mtoto huyo.

“Ila sijasema sasa Watanzania ndiyo mkazae na Wachina,” amesema

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata