MBUNGE AITAKA SERIKALI IBATILISHE NDOA ZA WALIO CHINI YA MIAKA 18

Mbunge wa Viti Maalumu, Kiteto Koshuma ameitaka serikali kutamka wazi kuwa wanawake walioolewa chini ya miaka 18, ndoa zao ni batili.

Koshuma ametoa kauli hiyo leo Aprili 18 bungeni wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2018/19.

Amesema sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1972 inakwenda kinyume makubaliano ya kimataifa.

Mbunge huyo ametoa masikitiko kuwa serikali haiwatendei haki wanaharakati ambao walipeleka kesi ya kupinga sheria hiyo mahakamani na wakashinda lakini serikali imekata rufaa.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata