MAMLAKA YA MAJI KAHAMA KUWASA YAPONGEZWA KWA KUANZA KULITUNZA BWAWA LA NYIHOGO.Viongozi wa mitaa inayozunguka bwawa la Nyihogo katika Halmashauri ya mji wa Kahama wameishukuru Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa mazingira mjini Kahama (KUWASA) kwa kuchukua hatua za utunzaji wa bwawa hilo lililokuwa limetelekezwa kwa muda mrefu.

Wakizungumza na wanahabari, diwani wa kata ya Nyihogo na diwani wa Muhungula wamesema wao kama wawakilishi wa wananchi wako tayari kushirikiana na mamlaka katika utunzaji wa bwawa hilo na kuiomba serikali kutenga bajeti ya utunzaji wa bwawa hilo kila mwaka.

Naye RAJABU RUHINDA, mzee aliyejitolea kutunza bwawa hilo amesema yeye alifika Kahama mwaka 1960 ambapo hapakuwa na mtu yoyote katika maeneo hayo na na ameiomba serikali kuendelea kulisafisha bwawa hilo ili kuweza kupata kina cha maji kilipofikia.

Akizungumza katika uzinduzi wa zoezi la upandaji wa miti katika bwala hilo hivi karibuni,  Mwenyekiti wa bodi ya KUWASA, Meja Mtsaafu BAHATI MATALA aliishukuru serikali kwa kulimilikisha rasmi bwawa hilo kwa KUWASA na kuahidi kulisimamia ili liweze kusaidia chanzo cha maji cha Ihelele kinapopata hitilafu.

KUWASA imetenga zaidi ya shilingi milioni 180 katika hatua za awali za utunzaji wa bwawa hilo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata