MAAFISA AFYA WA MAZINGIRA KAHAMA WATAKIWA KUWEKA SHERIA YA KUDHIBITI UMWAGAJI TAKA OVYO.


Imeelezwa kuwa Tatizo la  Mlundikano wa Uchafu  kwenye jirani na shule ya Msingi Kilima A, na B, halitakwisha endapo maofisa usafi wa mazingira kutoka halmashauri hawatatuamia sheria za kudhibiti umwagaji ovyo wa taka katika eneo hilo.

Akizungumza leo kwenye kipindi cha Raha ya Leo, Mwakilishi wa Kampuni ya Azani Logistics ambao ni wazabuni wa uzoaji wa taka mjini Kahama, WILLIUM SABAS amesema sheria ya halmashauri inapaswa itumike kuzuia wananchi kutupa ovyo taka katika eneo hilo.

Nao baadhi ya wananchi wameshauri halmashauri ya Mji wa Kahama kusimamia kikamilifu suala la usafi wa mazingira  huku wakiiomba kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama kufika katika shuleni hapo ili kunusuru wanafunzi wasipate madhara.

Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha   Usafi wa Mazingira katika Halmashauri ya Mji wa Kahama, MARTINE MASELE hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa madai kwamba amekuwa akilizungumzia mara kwa mara.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata