LIVERPOOL WAMEIOMBA MSAMAHA MAN CITY

Club ya Liverpool imelazimika kuiomba radhi club ya Man City kufuatia tukio la mashabiki wake kuamua kulishambulia basi la wachezaji wa Man City kwa kurushia chupa za maji wakati walipokuwa nje ya uwanja wa Anfield.

Liverpool walikuwa wenyeji wa Man City katika uwanja wa Anfield katika mchezo wa kwanza wa Club Bingwa Ulaya uliyomalizika kwa Liverpool kupata ushindi wa magoli 3-0, hivyo kitendo cha mashabiki kurushia chupa basi la Man City kimepingwa vikali.

Mashabiki wa Liverpool ambao walikuwa nje ya barabara za Anfield walianza kurusha miale ya moto na baadae ndipo walipoanza kurusha chupa za maji, kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameomba radhi pia.

“Kiukweli sielewi tulijaribu kwa kila namna kuzuia hiyo hali iliyojitokeza lakini kwa niaba ya Liverpool nalazimika kuomba radhi”>>>Klopp

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata