KIJANA AACHA SHULE NA KUAMUA KUFUGA NYOKA NDANI YA CHUMBA ANACHOISHI.

Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Peterson Ngure mkazi wa kijiji cha Kiandegwa nchini Kenya, ameshangaza watu baada ya kugundulika kuwa anaishi na nyoka wanne wenye sumu kali chumbani kwake.

Peterson ambaye ameacha shule akiwa darasa la sita, amesema huwa anatumia njia zake za maajabu kuwasiliana na nyoka hao, ambao amedai amewapata kwenye shamba la mpunga jirani na anapoishi.

Habari zinaeleza kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 20, amekuwa akiwachaji wananchi shilingi 20 za Kenya ambazo ni sawa na takriba shilingi 500 za Tanzania, kwa kila mtu anayetaka kuwaona nyoka hao.

Chifu msaidizi wa eneo hilo Julius Waweru amesema wanakusudia kumchukulia hatua kwa kitendo hiko ambacho si sahihi, na kwamba alishawahi kujaribu kumshawishi kijana huyo kurudi shule lakini juhudi zake ziligonga mwamba, bila kujua anajihusisha na shughuli hiyo ambayo ingeweza kuleta madhara kwa watu, iwapo nyoka hao wangewadhuru watu.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata