KICHANGA CHA SIKU 2 CHATUPWA KICHAKANI ISAKA KAHAMA.

Mtoto Mchanga anayekadiriwa  kuwa na umri wa siku 2 ameokotwa akiwa ametupwa kwenye kichaka kilichopo kandokando ya barabara kuu ya Isaka kuelekea Ushirombo katika kijiji cha sungamile wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Wakizungumza na Kijukuu Blog baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema tukio hilo limetokea april 28 mwaka huu asubuhi katika kijiji hicho ambapo mwanamke ambaye hajafahamika anadawa kutekeleza tukio hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa  kijiji cha Sungamile Ngusa Mayunga  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kuwa kuwa taka wananchi kutoa ushirikiano ili kumbaini aliyefanya unyama huo.

Jeshi la polisi kutoka kituo cha polisi Isaka Msalala  limefanikiwa  kufika katika  eneo la tukio  na kuamuru mtoto huyo kupelekwa katika hospitali ya mji wa Kahama ambapo hadi sasa anaendelea na matibabu.

Naye afisa wa jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia na watoto  wilayani Kahama mkoani Shinyanga  Koplo Ninael Kisagase amesikitishwa kutokea kwa kitendo  hicho cha kikatili huku akiiasa jamii kufichua vitendo   hivyo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata