JESHI LA NIGERIA LAFANIKIWA KUWAOKOA WATU 149 WAKIWEMO WATOTO NA WANAWAKE

Jeshi la Nigeria limeweza kuwaogoa watu 149 ambao walikuwa wameshikiliwa mateka na kundi la wapiganaji la Boko habarmu katika jimbo la Borno.

Wanawake na watoto 95 ambao walikuwa wakishikiliwa mateka katika kijiji cha Yerimari Kura wameweza kuokolewa baada ya jeshi la Nigeria kufanya operesheni katika eneo hilo ambalo lilikuwa linadhibitiwa na kundi la Boko haramu.

Wakati huo huo jeshi hilo limedai kuwaua wapiganaji watatu wa Boko haramu na wengine watano wamekamatwa na jeshi hilo wakati wa operesheni ya kuwaokoa watu waliotekwa na kundi hilo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata