HIKI NDICHO KILICHOWAPELEKA BABU SEYA NA WANAWE BUNGENI

Wanamuziki Nguza Viking maarufu Babu Seya wanawe Papii Kocha na Francis Nguza, leo wamealikwa Bungeni na kuhudhuria kikao cha Bunge leo.

Mara baada ya wasanii hao kutambulishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, ukumbi wa Bunge ulilipuka kwa kuwashagilia.

Babu Seya na wanawe hivi karibuni baada ya kutoka jela December 9, 2017 kwa msamaha wa Rais, wamekuwa wakialikwa sehemu mbali mbali za serikali, ikiwemo Ikulu na sehemu zingine za umma.

Babu Seya na wanawe walihukumiwa kifungo cha maisha kwa tuhuma za kulawiti na kubaka mwaka 2004 , na hatimaye neema ya Mungu kuwashukia pale Rais John Pombe Magufuli kuamua kuwasamehe na kuwaacha huru.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata