DC KAHAMA AWATAKA TRA KUSHIRIKIANA NA HALMASHAURI KUKUSANYA MAPATO.Serikali wilayani Kahama imeiagiza Mamlaka ya Mapato (TRA) katika mkoa wa kikodi Kahama kushirikiana na halmashauri katika ukusanyaji wa mapato ili kufanya mfumo wa ulipaji kodi kuwa rafiki kwa wananchi.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake jana mkuu wa wilaya ya Kahama, FADHILI NKURLU amesema sambamba na hilo TRA na halmashauri wanapaswa kutoa elimu ya mlipa kodi ili wananchi wapate uelewa juu ya umuhimu wa kulipa kodi mbalimbali.

Mkoa wa kikodi Kahama umeongoza katika ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2017/2018 katika mikoa ya kikodi nchini kwa kufanikiwa kukusanya shilingi BILIONI 5.4 ikiwa ni zaidi ya 150% ya lengo la kukusanya shilingi BILIONI 3.6.

WAKATI HUO HUO serikali wilayani Kahama imeiagiza halmashauri ya Msalala kuanza maandalizi ya kuhamia katika makao makuu yake yaliyopo Ntobo.

Mkuu wa wilaya ya Kahama, FADHILI NKURLU amesema  mpaka kufika mwanzoni mwa mwaka ujao wa fedha wa 2018/2019 idara zote zinatakiwa kuhamia Ntobo isipokuwa idara za kimfumo kama Teknolojia ya Mawasiliano (TEHAMA).

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata