BITEKO:WACHIMBA KOKOTO WANAWAZIDI WACHIMBA MADINI KULIPA MRABAHA

 NAIBU WAZIRI WA MADINI DOTTO BITEKO ALIYESIMAMA AKIONGEA NA WACHIMBAJI WADOGO KATIKA UKUMBI WA KAPAYA KAHAMA MJINI KATIKA SEMINA YA KUJIFUNZA USALAMA SEHEMU ZA KAZI.

KAHAMA
Serikali imesema bado kunautoroshaji wa  dhahabu  katika machimbo madogo kwenye mkoa wa Shinyanga hali ambayo inasababisha serikali kukosa mapato  mengi ambayo yangesaidia kuboresha huduma mbalimbali za jamii.

Hayo yameelezwa leo mjini Kahama na Naibu waziri wa Madini, DOTTO BITEKO wakati akizungumza na wachimbaji na wachenjuaji wa madini wa mkoa wa Shinyanga kwenye semina ya kujadili  usalama mahala pa kazi.

Amesema  kwa kipindi cha kuanzia mwezi  June 2016 hadi Februari 2018 wachimbaji wa mkoa wa  Shinyanga wameripotiwa kuzalisha kiasi cha  kilo  555.7 za dhahabu (sawa na shilingi milioni 45), kiwango ambayo amesema kipo chini ukilinganishwa na uzalishwaji.

BITEKO amesema wachimbaji wa madini wanazidiwa na  wachimbaji wa kokoto  na mchanga ambao  mwaka jana wamechimba tani milioni 15 na kulipa mrabaha shilingi wa biloni 7.5.

Wakizungumza na waandishi wa Habari baadhi ya wachimbaji na wachenjuaji  wameshauri kuongezwa udhibiti dhidi ya utoroshaji madini hayo pamoja na kupunguza  tozo na kodi mbalimbali kwa wachimbaji wadogo kwa manufaa ya serikali na wachimbaji hao.

MATUKIO KATIKA PICHA:


 KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WAKIWA MAKINI KUMSIKILIZA NAIBU WAZIRI WA MADINI DOTTO BITEKO HAYUPO PICHANI.

 BAADHI YA WACHIMBAJI WADOGO WAKIWA KATIKA SEMINA HIYO WAKIFUATILIA KWA MAKINI MAFUNZO YA USALAMA SEHEMU ZA KAZI.

 WACHIMBAJI WADOGO WAKIENDELEA KUFUATILIA HOTUBA YA NAIBU WAZIRI WA MADINI DOTTO BITEKO.

 BAADHI YA WACHIMBAJI WAKIMSIKILIZA NAIBU WAZIRI DOTTO BITEKO KATIKA SEMINA HIYO.

 WACHIMBAJI WADOGO WAKIENDELEA KUMSIKILIZA MH BITEKO HAYUPO PICHANI.MASOMO KUHUSU USALAMA SEHEMU ZA KAZI YAKIENDELEA HAPA BAADHI YA WACHIMBAJI WAKIENDELEA KUFUATILIA.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata