BITEKO AZITAKA HALMASHAURI KUTUNGA SHERIA NDOGO ZITAKAZOWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO.


Serikali  imeziagiza halmashauri  na serikali za mitaa  katika maeneo yote yenye wachimbaji wadogo wa madini  nchini kutunga sheria ndogo  zitakazokuwa na manufaa kwa  halmashauri na  wachimbaji wenyewe.

 Agizo hilo limetolewa jana  mjini Kahama na Naibu waziri wa madini, DOTTO BITEKO wakati akizungumza na Wachimbaji wa madini wa wilayani Kahama  kwenye semina juu ya  Usalama  na afya mahala pa kazi.

Amesema suala la Wachimbaji wadogo ni mtambuka   hivyo ni lazima kuweka sheria zitakazokuwa rafiki kwao na hivyo kuongeza uchumi wao na wa taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri BITEKO amesema serikali imeongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato kwenye sekta ya madini  kutoka wastani wa shilingi bilioni  178 hadi 200 kwa mwaka hadi shilingi bilioni 203.

Akizungumzia suala la Usalama na afya  mahala pa kazi, Meneja  wa  Baraza la wakala wa usalama mahala pa kazi, (OSHA)  mkoa wa Shinyanga, MJAWA MOHAMED amesema  lengo ni kuwajengea uelewa wachimbaji katika kujilinda na kuzingatia usalama  na afya zao kazini.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata