BENKI YA TPB YATOA MSAADA WA MADAWATI KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYANSHIMBI WILAYANI KAHAMA.


MKURUGENZI WA MASOKO WA BENKI YA POSTA NCHINI (TPB), HENRY BWOGI KULIA AKIMKABIDHI DAWATI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA ANDERSON MSUMBA MWENYE MIWANI KUSHOTO

KAHAMA
Jamii wilayani Kahama mkoani Shinyanga imetakiwa kushiriki kikamilifu katika kuchangia miradi ya maendeleo ya shule ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kusaidia uwepo wa mazingira rafiki kwa wanafunzi.

Wito huo umetolewa leo  mjini Kahama na Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya Posta nchini (TPB), HENRY BWOGI   wakati wa kukabidhi madawati 50 na viti 50  vyenye thamani ya shilingi milioni nne kwa shule ya sekondari Nyashimbi, mjini Kahama.

BWOGI amesema   kama wazazi watasimama kidete kutoa michango ya hali na mali kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu shuleni, ni wazi kwamba changamoto zinazojitokeza shuleni zitapungua.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, ANDERSON MSUMBA pamoja na kuipongeza benki ya TBP amesema halmashauri hiyo imejipanga kuboresha miundombinu shuleni.

Kwa upande wake meneja wa benki wa TPB tawi la Kahama Jumanne Wagana ambaye ni mwenyeji na mratibu wa zoezi hilo,amesema kuwa benki ya TPB itaendelea kuchangia katika miradi mbali mbali ya maendeleo na kutoa wito kwa jamii kushirikiana na benki hiyo katika mambo mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.

Diwani wa Kata ya Mhongolo ilipo shule ya hiyo ya Sekondari   Nyashimbi, MICHAEL MIZUBO amesema shule hiyo ina changamoto nyingi hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kutoka kwa wadau ili kutatua changamoto  hizo.

Nao baadhi ya wanafunzi walioongea na kijukuu Blog wamesema kuwa msaada huo utawapunguzia kero ya upungufu wa madawati uliopo na kutoa wito kwa taasisi zingine za kifedha kuwasaidia viti na meza ikiwa ni pamoja na vumba vya madarasa kwani uhitaji bado mkubwa.

Benki ya TPB imetoa msaada wa viti na meza Hamsini vyote vikiwa na Gharama ya shilingi Milioni nne.

MATUKIO KATIKA PICHA:
MKURUGENZI WA MASOKO WA BENKI YA POSTA NCHINI (TPB), HENRY BWOGI AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI PAMOJA NA VIONGOZI WA HALMASHAURI YA KAHAMA MJINI KATIKA ZOEZI LA KUKABIDHI MADAWATI. BAADHI YA MADAWATI YALIYOTOLEWA NA BENKI YA TPB YAKIWA KATIKA UWANJA WA SHULE YA SEKONDARI NYANSHIMBI.

 WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NYANSHIMBI WAKIIMBA WIMBO WA SHULE KATIKA HAFLA YA KUKABIDHIWA MADAWATI HAYO ILIYOFANYIKA KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYANSHIMBI.

  WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NYANSHIMBI WAKIIMBA WIMBO WA SHULEMENEJA MAHUSIANO WA BENKI YA TPB NOVES MOSES AKIWASALIMIA WANAFUNZI NA WATUMISHI WA HALMASHAURI KATIKA TUKIO LA KUKABIDHI VITI NA MEZA.

 MENEJA WA BENKI TAWI LA SHINYANGA AMON KAMUGISHA AKIJITAMBULISHA NA KUZUNGUMZA MACHACHE KATIKA TUKIO LA KUKABIDHI MEZA NA VITI LILILOFANYIKA KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYANSHIMBI WILAYANI KAHAMA MKOANI SHINYANGA.

 MENEJA WA BENKI YA TPB TAWI LA KAHAMA JUMANNE WAGANA  AKIJITAMBULISHA NA KUSEMA MACHACHE KATIKA TUKIO HILO LA KUKABIDHI VITI NA MEZA.

 AFISA MAENDELEO YA JAMII KATIKA KATA YA MHONGOLO BI HILDA AKISALIMIA KATIKA TUKIO HILO LA KUKABIDHI VITI NA MEZA KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYANSHIMBI.

 DIWANI WA KATA YA MHONGOLO MICHAEL MIZUBO AKITOA SHUKRANI KWA UONGOZI WA BENKI YA TPB KWA KUWAWEZESHA KUPATA MSAADA HUO WA VITI NA MEZA 50 

 AFISA ELIMU WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA AKIELEZA  HALI YA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA KWA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA NA SHULE YA SEKONDARI NYANSHIMBI.

 MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA USHETU ANDERSON MSUMBA AKIZUNGUMZA KATIKA TUKIO HILO LA KUKABIDHIWA VITU LILILOFANYIKA KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYANSHIMBI.

 BAADHI YA WALIMU WA SHULE YA SEKONARI NYANSHIMBI PAMOJA NA WATUMISHI WA  HALMASHAURI YA KAHAMA MJINI WAKIWA KATIKA TUKIO LA KUKABIDHI MEZA NA VITI 50 VILIVYOTOLEWA NA BENKI YA TPB 

 MENEJA WA BENKI YA TPB TAWI LA KAHAMA JUMANNE WAGANA KUSHOTO PAMOJA NA MENEJA WA TAWI LA TPB SHINYANGA AMON KAMUGISHA KULIA WAKIFURAHIA JAMBO WAKIWA WAMEKAA NA WANAFUNZI KATIKA MADAWATI WALIYOTOA.

 MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA ANDERSON MSUMBA MWENYE MIWANI AKITETA JAMBO NA MMOJA WA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NYANSHIMBI WAKIWA WAMEKAA KATIKA MADAWATI YALIYOTOLEWA NA BENKI YA TPB.

 NYUSO ZA FURAHA ZIKIWA ZIMETAMALAKI BAADA YA ZOEZI LA MAKABIDHIANO KUKAMILIKA HAPA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA AKISISITIZA JAMBO KWA WANAFUNZI AMBAO WATATUMIA VITI NA MEZA HIZO.

 VIONGOZI WA KATA YA MHONOLO,WAWAKILISHI WA BENKI YA TPB,WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA PAMOJA NA WANAFUNZI WAKIWA WAMEKAA KATIKA MADAWATI HAYO ISHARA YA UZINDUZI RASMI WA MATUMIZI YA VITI NA MEZA HIZO.

MENEJA WA BENKI YA TPB TAWI LA KAHAMA JUMANNE WAGANA AMABYE NDIYE MWENYEJI WA ZOEZI LA UTOAJI VITI NA MEZA HIZO AKIWA ANATOKA ENEO LA TUKIO MARA BAADA YA KUKAMILISHA ZOEZI.
SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata