ASKOFU KAKOBE ATAKIWA KURIPOTI UHAMIAJI

 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amesema ameitwa kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji siku ya Jumatatu, Aprili 9, 2018.


Akizungumza lleo Jumamosi Aprili 7, 2018 Askofu Kakobe amesema ataitikia wito huo.

“Wamenieleza kuwa wananiita kwa sababu ya mahojiano hivyo nitakwenda tu hakuna shida. Wameniita Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam,”amesema Kakobe

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata