ALIYEJIUZULU UDIWANI CHADEMA, AVULIWA UANACHAMA

Katibu wa Chadema, Kanda ya Iringa Mjini, Suzana Mgonokulima, ametangaza kumvua uanachama  aliyekuwa diwani wa chama hicho, Kata ya Gangilonga, Dady Igogo. Igogo pia alikuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa.

Katika taarifa iliyotolewa leo Aprili 28, imeelezwa kuwa Igogo amevuliwa uanachama kwa kuwa alikisaliti chama kwa kujivua nafasi ya unaibu meya na baadaye udiwani.

“Ndugu Igogo kwa muda mrefu amekuwa na mwenendo usioendana na itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za chama,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema kamati tendaji ya jimbo katika kikao chake cha dharura kilichoketi Aprili 24 mwaka huu kiliadhimia Igogo avuliwe ujumbe wa kamati tendaji ya jimbo, kwa kwenda kinyume na katiba ya chama kanuni na maadili.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Igogo amevuliwa uanachama kuanzia leo Aprili 28 kama ilivyokubaliwa na wajumbe wa kamati.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata