ALI CHOKI AWATUPIA LAWAMA WATANGAZAJI WENYE UMRI MDOGO KUUWA MZIKI WA DANSI.

Msanii Mkongwe wa muziki wa dansi nchini Tanzania, Ali Choki ametaja sababu zilizoupoteza kwenye ramani muziki wa dansi nchini Tanzania.

Ali Choki akiongea na Waandishi wa Habari jana Aprili 07, 2018 kwenye uzinduzi wa Respect Barber Shop amesema kuwa sababu kubwa ni umri wa watangazaji wengi kwenye vipindi vya burudani kuwa mdogo na wengi wao wanapendelea kucheza muziki wa Bongo Fleva sana kwani kipindi muziki wa dansi unatamba wengi wao walikuwa ni wadogo.

Akitoa sababu nyingine ya kupotea kwa muziki wa dansi ni uwezo wa kifedha wa kutengeneza video kali ambazo zingewafanya watu wengi wavutiwe kuangalia kazi za muziki huo.

Ali Choki amesema kuwa amejipanga kuurejesha muziki huo kwa upande wake ameahidi kufanya kolabo na msanii mkubwa wa Bongo Fleva na kutengeneza video nzuri ili kuvutia kizazi kipya cha Bongo Fleva

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata