WIMBO WA KIBAMIA WAMPONZA ROMA MKATOLIKI AFUNGIWA MIEZI SITA.

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imemfungia mwanamuziki Ibrahim Musa ‘Roma Mkatoliki’ asishughulishe na sanaa kwa miezi sita.
Msanii Emannuel Elibariki 'Nay wa Mitego' amepewa onyo kali kuhusu maudhui ya nyimbo zao.
Msanii Roma amefungiwa kutoimba wala kujihusisha na sanaa kutokana na kuimba wimbo wa Kibamia ambao hauna maadili.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amewaeleza waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuwa, hakuna kituo chochote cha redio wala runinga kupiga wimbo wa Roma mpaka atakapomaliza adhabu hiyo.
Amesema hiyo ni hatua ya kwanza na kwamba wataendelea kufungia baadhi ya nyimbo pamoja na wasanii ambao wataimba kwa kukiuka sheria na maadili ya Baraza la Sanaa Tanzania (Basata).
Kwa mujibu mujibu wa Shonza, amezungumza na Basata kuhakikisha kila msanii anayekiuka maadili ya baraza hilo anachukuliwa hatua papo hapo, huku akisisitiza kuwa wasanii lazima wazingatie miiko na maadili.
Kuhusu Nay, amepewa onyo na wizara hiyo kutokana na nyimbo zake Pale kati patamu na Maku makuz.
“Nay tulimwita na alifika kujitetea tofauti na wasanii wengine, hivyo tumempa onyo”.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata