WALIOMCHEZEA RAFU RAIS NKURUNZINZA KWENYE SOKA WAFUNGWA JELA

Watu wawili wamekatwa na kufungwa jela baada ya kumchezea rafu Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza katika mchezo wa kirafiki uliokuwa dhidi ya timu yake na wapinzani.

Nkurunzinza ambaye alikuwa na kikosi chake cha Haleluya FC, Februari 3 2018 walikuwa wakicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kimbere FC iliyopo Kaskazini mwa nchi hiyo ya Burundi.

Katika mchezo huo, Kiremba FC ilikuwa na wachezaji ambao baadhi ni wakimbizi kutoka Congo waliokuwa hawajui kama wanacheza na Rais wa Burundi hivyo walikuwa wakimchezea rafu kila muda.

Kitendo cha kumchezea rafu Rais huyo, kilichukuliwa kama njama za kutaka kuhatarisha afya ya Rais Nkurunziza hivyo Serikali ikachukua maamuzi ya kuwafunga jela.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata