WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU (TSF) INATARAJIA KUPANDA MITI ELFU 34 WILAYANI KAHAMA.Jumla ya miche ya miti 34,000 inatarajiwa kupandwa katika eneo la mita za maraba 21.25 wilayani KAHAMA mkoani SHINYANGA na WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU wilayani humo (TFS) katika kipindi cha mwezi march 2018.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji miti uliofanyika katika chanzo cha maji cha NYIHOGO, kaimu meneja wa misitu wa wilaya MOHAMED DOSSA amesema lengo la wakala huo ni kuhakikisha Kahama inakuwa ya kijani.

Akizungumza katika uzinduzi huo mkuu wa wilaya ya kahama FADHILI NKURLU ameiagiza mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini KAHAMA KUWASA kuhakikisha inakifufua chanzo cha maji NYIHOGO ili kihudumie wananchi wakati maji yanapokatika.

Naye mwenyekiti wa bodi ya maji KUWASA BAHATI MATALA ameishukuru serikali kwa kulirudisha eneo hilo rasmi chini ya KUWASA na ameahidi kulisimamia na kwamba tayari wamepanda miti 6100 katika katika juhudi za kupambana na uharibifu mkubwa uliosababishwa na shughuli za kibinadamu.

Takwimu zinaonesha kuwa TANZANIA bara ina jumla ya hekta milioni 48.1 za misitu ambayo ni sawa na 55% ya eneo lote la TANZANIA bara.

Wakala wa huduma za misitu TANZANIA ni wakala wa serikali ambao umeanzishwa kwa tangazo la serikali namba namba 269 la 2010 kwa ajili ya kusimamia misitu yote ya kitaifa, maeneo ya ufugaji nyuki pamoja na misitu iliyopo katika maeneo ya wazi.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata