UKWELI KUHUSU TIMU YA SIMBA FC KUAZIMA BASI LA AZAM FC

  Klabu ya soka ya Azam FC imeweka wazi kuwa haina mahusiano yoyote na timu ya Al Masry, ambayo imetua nchini leo kwa ajli ya kucheza na Simba huku Simba ikitumia Basi la Azam Fc kutoka Uwanja wa ndege kuelekea hotelini.
Akiongea na wanahabari msemaji wa Azam FC Jaffary Idd Maganga amesema kuwa kutoa Basi ni sehemu ya biashara ya klabu hivyo kwa timu yoyote ambayo inahitaji huduma hiyo ifuate tu taratibu zote na itapata Bus.
''Basi ni sehemu ya biashara ya timu na siyo mara ya kwanza kutumika hata timu ya taifa huwa inatumia mara nyingi tu kama ilivyo kwa uwanja wetu, na uongozi wa Simba umeandika barua kwa CEO na wamepewa lakini hatuna mahusiano na Al Masry'', amesema.
Al Masry imetua leo nchini tayari kwa mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya wenyeji wao Simba siku ya Jumatano Machi 7 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata