UBOVU WA BARABARA ENEO LA MHONGOLO KAHAMA WASABABISHA MADEREVA BAJAJI KUFUNGA BARABARA KWA SAA MBILI.Ubovu wa barabara ya muda inayotumika kusafirisha abiria kutoka Mjini Kahama kwenda Mtaa wa Mhongolo  umesababisha   baadhi ya waendesha   pikipiki za magurudumu matatu (Bajaji) kufunga barabara hiyo kwa zaidi ya saa mbili, kushinikiza serikali iifanyie ukabarabati.

Baadhi ya waendesha Bajaj wamesema wamelazimika kufunga barabara ili kufikisha kilio chao kwa serikali kwani wamekuwa wakipata usumbufu kutokana na  ujenzi wa barabara hiyo ya Mhongolo.

Jeshi la  Polisi wilayani Kahama kupitia mkuu wa kitengo cha Usalama barabarani, DESDERY KAIGWA limewaelekeza Madereva hao wa Bajaj kufuata taratibu kwa kupeleka malalamiko yao kwa  viongozi wanaohusika kuliko kufunga barabara kwani  kufanya hivyo ni kuvunja sjeria. 

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa barabara TANROADS mkoa wa Shinyanga, MIBARA NDIRIMBI amesema hali hiyo inatokana na  kutokuwepo kwa mipango miji  bora hali inayosababisha  maji kuharibu miundombinu hiyo na kwamba amemuagiza  mkandarasi kuboresha barabara ya muda.

Barabara hiyo ya muda  inayotoka Mjini Kahama kwenda Mhongolo inatumika kutokana na  kuwepo kwa ujenzi wa barabara  yenye kiwango cha Lami kutoka Mjini Kahama hadi Mhongolo.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata