SERIKALI KUONDOA MITI YA MIKARATUSI KATIKA MLIMA KILIMANJARO

Na ferdinand shayo,arusha.
Serikali mkoani kilimanjaro itaanzisha kampeni ya kuiong'oa miti yote aina ya mikaratusi na kuua mizizi yake ambayo inakwenda kina kirefu ardhini na kunyonya maji mengi na hivyo  kuchangia ukame na kukauka  kwa vyanzo vya maji na mito iliyoko katika hifadhi ya  mlima kilimanjaro..
Mkuu wa mkoa huo bi anna mghwira ametangaza uamuzi huo katika ibada ya maombi maalum ya kuliombea taifa  liendelee kuwa la amani  na rais john magufuli  kwa kazi nzuri anayoifanya  na kuyashirikisha madhehebu yote ya dini na waumini wake yaliyoandaliwa na ofisi yake kwenye uwanja wa mashujaa mjini moshi.
Bi mghwira amesema, miti hiyo ambayo imeota kando ya mito na vyanzo vya maji imegunduliwa kuwa ni moja ya sababu  ya kukauka kwa mito  na vyanzo hivyo na amewataka viongozi wa dini kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuing'oa miti hiyo kwa maelekezo yatakayotolewa na wataalam ili pia kuuhifadhi mlima k'njaro.
Askofu isaack amani wa kanisa katoliki jimbo la moshi amewataka watanzania kuwalea watoto wao kwa misingi ya  maadili mema ili baadae taifa liwe na raia wema na viongozi bora ambao watapambana na rushwa, ufisadi na maovu yote katika jamii ili nchi iendelee kuwa na amani.
kiongozi wa madhehebu ya hindu bw dinesh shah amempongeza rais john  magufuli kwa kazi kubwa ya kuleta maendeleo ya wananchi katika nyanja mbali mbali ikiwemo azma yake ya kuwa na tanzania ya viwanda  bila kujali itikadi ya vyama vya siasa na madhehebu ya dini.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata