OFISA WA SERIKALI AJIFUNGUA WATOTO WANNE KWA MPIGO

Ofisa Tarafa wa Kibamba, wilayani Ubungo, Beatrice Mbawala amejifungua watoto wanne kwa mpigo katika Hospitali ya Agha Khan, jijini Dar es salaam.


Beatrice amejifungua watoto hao wakiwa njiti mwezi mmoja uliopita.


Akizungumza hospitalini hapo, Machi 3, baba wa watoto hao, Julius Mbawalla amesema familia yake ina furaha kupokea watoto wanne na kwamba jukumu lake kubwa ni kuhakikisha mkewe anapata huduma muhimu ili aweze kumudu kuwanyonyesha.


Daktari Bingwa wa Watoto katika hospitali ya Agha Khan, Dk Mariam Mgonja amesema afya za watoto zimeimarika na tayari wameruhusiwa kwenda nyumbani.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata