NABII SHILLA ASEMA HAJAFUNGIWA HUDUMA

Nabii Daniel Daniel Shilla
KIONGOZI wa Kanisa la Bethel Ministry nchini,Nabii Daniel Daniel Shilla anayedaiwa ana utajiri mkubwa wa fedha ambaye habari zilienea kwamba amefungiwa kutoa huduma,ameibuka na kukanusha kuwa hajafungiwa.

Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar, Nabii Shilla alisema ni kweli huduma yake ilikuwa na matatizo na alikwenda Dodoma kushughulikia tatizo hilo ambalo alisema aliaambiwa na askofu wake, Peter Mlai kwamba anamfungia huduma kutokana na kujihusisha na siasa “Nilikwenda Dodona na kuonana na maofi sa wa serikali ambao waliniambia kuwa nilifanya kosa la kumtabiria mgombea wa ubunge wa Chadema katika Jimbo la Kinondoni kwamba atashinda katika uchaguzi, ni kweli nilifanya hivyo. “Lakini niliwaelewesha kwamba nabii anapotoa unabii wake huwa anaoneshwa.

Hivyo sijafungiwa na kanisa halijafungwa. Niliwaambia viongozi wa serikali kwamba sijawahi kumtukana rais au serikali na huwa nawaombea na serikali inafanya kazi vizuri sana isipokuwa kuna vitu vidogovidogo vikitokea huwa sisiti kusema kwa sababu nikikaa kimya nitakuwa mnafi ki.

“Kwa mfano, anakuja muumini wako analalamika kuwa amevunjiwa nyumba na suala lipo mahakamani,hapo ni lazima utamsikiliza na utasema, ukikaa kimya utakuwa mnafi ki,” alisema Nabii Shilla.Alisema hata mwaka 2020 utakapofi ka (wakati wa uchaguzi mkuu), hataacha kueleza kile ambacho ataoneshwa na Mungu kwa kuwa hiyo ndiyo kazi yake.

Hivi karibuni Nabii Shilla alidai kuwa kanisa lake limefutiwa usajili baada ya yeye kutabiri kupitia facebook kwamba mgombea wa ubunge kwa tiketi ya Chadema (Salum Mwalimu) Jimbo la Kinondoni atashinda.

Hata hivyo Nabii Shilla alisema yeye aliongozwa na Mungu kutoa unabii ule hivyo akatakiwa kuripoti kwenye Ofi si ya Msajili wa Vyama mjini Dodoma kesho, hivyo atakwenda kuitikia wito hata kama ni kwa miguu.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata