MWENYEKITI MPYA WA UMOJA WA VYAMA VYA WAKULIMA WA TUMBAKU TANZANIA,APANGA KUTUMIA KALENDA KUBORESHA ZAO HILO.


 EMMANUEL CHEREHANI

KAHAMA
Umoja wa Vyama vya Wakulima wa Tumbaku nchini (TCJE) umesema kuwa utahakikisha unafuata kalenda ya zao la Tumbaku ili kudumisha zao hilo katika mikoa yote ya kitumbaku nchini kwa manufaa ya wakulima na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa leo na mwenyekiti wa Umoja huo, EMMANUEL CHEREHANI katika mahojiano na Kahama Fm ofisi kwake kuhusu mikakati ya umoja huo katika kulikomboa zao la Tumbaku nchini.

CHEREHANI amesema kuwa zao la Tumbaku likilimwa kwa kufuata Kalenda yake hususan katika kuwahisha pembejeo, madawa na kuwa na masoko ya uhakika ili wakulima wauze tumbaku ikiwa na ubora, litaleta manufaa makubwa kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.

CHEREHANI amesema sanjari na kushirikiana na Serikali  kwa kufuata taratibu na Sheria zote za Vyama vya Ushirika, Umoja huo wa vyama vya wakulima wa Tumbaku nchini utaendelea kujadiliana na taasisi za kifedha ili kupunguza riba kwa wakulima wa Tumbaku.

Umoja wa vyama vya wakulima wa Tumbaku Tanzania (TCJE) unaundwa na vyama vikuu vinane vya Ushirika vya Tumbaku kutoka katika mikoa ya Kitumbaku ya Kahama, Tabora, Chunya, Mpanda, Manyoni, Songea, Kigoma na Iringa.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata