MOURINHO, RONALDO NA KOCHA WA MONACO WASHINDA TUZO URENO

Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho usiku wa jana katika mji wa Lisbon wamefanikiwa kushinda tuzo zilizotolewa na shirikisho la soka la Ureno.

Ronaldo, 33, ameshinda tuzo hiyo mwaka huu kwa mara ya tatu mfululizo kwa kuwabwaga wachezaji wenzake wengine wa Ureno akiwemo Bernardo Silva (Manchester City) na golikipa Rui Patricio (Sporting CP).


Naye Mourinho ameshinda tuzo ya Vasco de Gama kutokana na kufanya kazi yake kwa ubora na majukumu yake kama ubalozi wa Ureno.

Wakati huo huo kocha wa klabu ya AS Monaco ya Ufaransa, Leonardo Jardim ameshinda tuzo ya kocha bora kwenye upande wa soka wa wanaume.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata