MLIPUKO WAUA WACHINA WAWILI WAKICHIMBA DHAHABU GEITA

Raia wawili wa China wamefariki dunia na mlipuko wakati wakipasua mwamba kwa ajili ya kuchimba dhahabu katika mgodi unaomilikiwa na Mayala Ngweso, uliopo kijiji cha Nyamtondo wilayani Geita.
Akizungumza leo Jumanne Machi 27, 2018, kamanda wa polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba chanzo ni uzembe baada ya Wachina hao kulipua mwamba bila kuchukua tahadhari.
Amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Li Shaobin (44) na Qian Zhaorang (49) na kwamba, miili yao imehifadhiwa Hospitali ya Makoye iliyopo mjini Geita na kwamba walikuwa wakiishi nchini kihalali.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata