MKURUGENZI WA SHULE YA SEKONDARI DON BOSCO DIDIA PADRI RICHARD MTUI AFARIKI DUNIA


Padri Richard Mtui enzi za uhai wake

Mkurugenzi wa shule ya sekondari Don Bosco Didia iliyopo katika wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga ,Padri Richard Mtui amefariki dunia katika ajali ya gari mkoani Singida.

Inaelezwa kuwa Padri Mtui amefariki leo Ijumaa Machi 30,2018 saa 11 alfajiri baada ya gari aina ya Noah aliyokuwa anasafiria kutoka Moshi kugongana na lori mkoani Singida.

Akizungumza na Malunde1 blog kwa simu,Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kubainisha kuwa taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuja Shinyanga kwa ajili jumuiya ya Don Bosco na kanisa kwa ujumla kuaga mwili wa marehemu.

"Alikuwa anatoka Moshi kwenye msiba wa ndugu yake,Mwili wake bado upo Singida, utasafirishwa kuja Don Bosco kwa ajili ya kumuaga mpendwa wetu,tumepoteza mtu muhimu,alikuwa mnyenyekevu na mtu wa kujituma sana katika kazi",amesema Askofu Sangu.

Mungu ailaze mahali pema mbinguni roho ya marehemu Padri Richard Mtui.Amina.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata