MABATI YA LEMBELI YAZUA KIZAA ZAA KAHAMA,MWALIMU MKUU AVULIWA MADARAKA AKITUHUMIWA KUUZA MABATI 20 KATI YA 90.


Salvatory Calvin-Kijukuu Blog

KAHAMA
Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga imemvua madaraka mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Ifunde, DAUD WARIOBA kwa Tuhuma ya kuuza Mabati 20 kwa kushirikiana na Kamati ya shule hiyo kinyume na utaratibu.

Uamuzi huo umetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo MICHAEL MATOMORA kwenye mkutano wa maalumu wa kijiji ulioitishwa kwaajili ya kujadili Tuhuma ya wizi wa mabati ya shule.

Amesema Mtumishi yeyote aliyepewa dhamana ya kusimamia Taasisi ya Ummaa haruhusiwi kuuza mali za umma hivyo ofisi yake itamtuma mkaguzi wa ndani kwaajili ya kukagua mali hizo.

Hoja hiyo imeibuliwa na wananchi wa kijiji hicho baada ya kukamata mabati hayo kwa MABULA NDIIKWA aliyeyanunua katika shule hiyo kinyume na utaratibu ulioainishwa.

Naye Mwalimu DAUDI WARIOBA amekiri Tuhuma hiyo kwenye mkutano huo kwa madai kwamba alifuata taratibu za uuzaji mabati hayo 20 kwa kuwashirikisha wajumbe wa kamati ya shule hiyo.

Kwa upande wake aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama JAMES LEMBELI amesikitishwa na Taarifa hiyo na kutoa wito kwa uongozi wa Halmashauri hiyo kufuatilia mabati na fedha alizozitoa katika shule za msingi Bulima, Ilekebu,na Zahanati ya Butende kama zimetumika kwa usahihi.

Mabati hayo 20 ni miongoni mwa mabati 90 yaliyotolewa katika shule hiyo kwaajili ya kuezekea nyumba ya walimu na mwaka 2014 kutoka Mfuko wa jimbo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata