LEMA : SI AJABU UKASIKIA SILAHA ILIYOMUUA AKWILINA IPO NYUMBANI KWA KIONGOZI WA CHADEMA


Machi 30, 2018 Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameongea kuhusu taarifa iliyotolewa na Kamanda wa kanda maalum ya DSM Lazaro Mambosasa kuhusu silaha iliyotumika kumuua Akwilina kuwa bado haijajulikana na wanaendelea na upelelezi.

Lema kupitia akaunti yake ya Twitter ameandikia kuwa ameitafakari kauli ya Mambosasa kuhusu tukio la Akwilina juu ya silaha iliyotumika.

“Nimeitafakari kauli ya Mambosasa inayohusu tukio la Akwilini kuhusu silaha iliyotumika, bila shaka kuna dhambi kubwa inapangwa nawasihi Wana CHADEMA kuwa makini wakati huu kwani si ajabu ukasikia kuwa Ile silaha iliyotumika kumuua Akwilini imekutwa nyumbani kwa Kiongozi wa CHADEMA” -Lema

Nimeitafakari kauli ya Mambosasa inayohusu tukio la Akwilini kuhusu silaha iliyotumika,bila shaka kuna dhambi kubwa inapangwa nawasihi WanaChadema kuwa makini wakati huu kwani si ajabu ukasikia kuwa Ile silaha iliyotumika kumuua Akwilini imekutwa nyumbani kwa Kiongozi wa CHADEMA

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata