JPM; WAKANDARASI TUMIENI BIDHA ZINAZOZALISHWA NCHINI.

Related image
VIONGOZI na Makandarasi wazawa wanaopata kazi za kutandika mabomba katika miradi mbalimbaali inayotolewa na serikali wahakikishe kuwa wanatumia bidhaa za ndani kabla ya kutumia bidhaa za nje ili kuinua uchumi na kuongeza ajira kwa watanzania.
Ukitumia bidhaa za ndani unasaidia kutengeneza ajira kwa wazawa kuliko unapotumia bidhaa za nje ambapo unakuwa unatengeneza ajira kwa watu wa nje nakuwataka wamiliki wa viwanda vinavyotengeza bidhaa hiyo bidhaa kwa ubora unaotakiwa ili kulinda soko la ndani.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr, John Magufuli Maguli aliyabanisha hayo jana wakati akifungua kiwanda cha utengezaji wa mabomba ya plastiki,Mabati pamoja chuma kinachomilikiwa na Kahama Oil mill  kilichopo katika Mji wa kaahama.
Magufuli alisema kuwa kila mkandarasi hapa nchini anatakiwa kutumia bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini katika shughuri yake nakuongeza bidhaa zoinapoisha na shughuli zake bado zinaendelea anatakiwa kupata kibari cha kuagiza bidhaa kutoka nje.
“Kila mtanzania anatakiwa kuwa mzalendo kwa kupenda chakwake nasio kupenda bidhaa vinazotengeneza nje hali ambayo haingezi kuongeza ajira kwa watanzania na kukuza uchumi wanchi,badala yake tunakuwa tunawatengezea ajira watu wanje” alisema Magufuli.
Hata hivyo alizitaka taasisi za fedha yakiwemo  mabenki  kuhakikisha yanapunguza riba kwa wafanyabiashara na kuongeza kuwa  awali mabenki mengine yalikuwa  yanatoza riba kubwa  mpaka asilimia 25  hali ambayo wawekezaji wa viwanda  wanashidwa kujiendesha na kujikuta yanapata hasara huku akisema kwa sasa jumla ya viwanda 3600  tayari  vimekwisha  funguliwa nchini .
Katika hatua nyingine Dr, pombe John Magufuli amewataka   wawekezaji  kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini hususani  madini ya chuma  hali itakayowafanya  kuzalisha bidhaa zao kwa faida kubwa kuliko kuendelea kutumia malighafi kutoka nje.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwawanda cha Kahama Oil Mill Mhoja Nkwambi alisema kuwa kiwanda kilianzishwa mwaka 2002 nakutoa ajira 720 huku 120 zikiwa ajira za kudumu na 600 zikiwa ajira za muda mfupi kulingana na upatikanaji wa malighaf
Alisema kuwa amekuwa akipata changamoto za uzaji wa bidhaa anazozalisha kutokana na bidhaa zinazotengenezwa nje kuingia kwa wingi nakupelekea bidhaa zinazotengezwa ndani kukosa soka hata kama zinakidhi ubora.
Nkwambi aliendelea kusema kuwa serikali ithamini bidhaa zinazotengenezwa ndani badala ya kutoa kipaumbele kwa bidha zinazotoka nje ya nchi na kuvilinda viwanda vya ndani ili viweze kujiendesha na kupata mikopo ya riba fuu kutoka katoka katika mabenki na tasisis mbalimbali za kifedha.
Pia Mkurugenzi huyo aliiomba serikali kumsaidia kupata soko la mabomba ya plasti,Mabati na vyuma hapa nchini ili wanunuzi waache kuagiza bidhaa hizo kutoka nje nahali hiyo itasida kuvilinda viwanda katika ushindani wa kibishara katika masoko ya ndani na nje.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata