HUYU NDIYE KIJANA ANAYEJIPIGA SELFIE '200' KWA SIKU

Kijana Junaid Ahmeid amekiri kuwa amepata uraibu wa kujipiga picha na kisha kuzituma katika mitandao ya kijamii.

Junaid raia wa Uingereza aliyehojiwa na Shirika la Utangazaji la BBC, alisema ana wafuasi 50,000 katika mtandao wa kijamii wa Instagram na hujipiga picha 200 kwa siku.

Anasema hujipiga picha kwa uangalifu na kuzituma kwenye mtandao wake wa kijamii ili watu wengi wabonyeze kitufe cha kuzipenda (likes)  na endapo atapata ‘likes’ chini ya 600 huifuta picha hiyo.

“Nikiweka picha katika dakika ya kwanza au ya piki, najua kabisa itapata ‘likes’ 100 na ninafurahi, simu yangu inachangamka,” amesema

Junaid anakiri kuwa kupenda kwake kujipiga picha wakati mwingine humkosanisha na marafiki na ndugu

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata