EMMANUEL CHEREHANI ACHAGULIWA KWA KURA ZOTE ZA NDIYO KUWA MWENYEKITI WA VYAMA VIKUU VYA TUMBAKU TANZANIA.MWENYEKITI WA VYAMA VIKUU VYA WAKULIMA WA TUMBAKU TANZANIA EMMANUEL CHEREHANI


MOROGORO
Wakulima wa zao la Tumbaku nchini wametakiwa kuwa na umoja na ushirikiano ili kuimarisha ubora wa zao hilo hali itakayosaidia kuinua uchumi wa nchi na na mtu mmoja mmoja katika kufikia uchumi wa viwanda.

Wito huo umetolewa jana mjini Morogoro na mwenyekiti wa vyama vikuu vya wakulima wa Tumbaku Tanzania Emmanuel Cherehani mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa kumtafuta Mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa Muungano huo.

Katika uchaguzi huo Cherehani alipata kura zote za ndiyo kutoka kwa wajumbe 40 wa vyama vyote vinane ambapo kila chama kilikuwa na wajumbe watano huku nafasi ya makamu mwenyekiti ikichukuliwa na Gulila Mwakosya kutoka chama cha CHUTCU kilichopo Chunya mkoani Mbeya.

Cherehani amesema kuwa ili zao la tumbaku lilete tija kwa wakulima na taifa kwa ujumla ni vyema viongozi na wakulima wawe na Lugha moja huku akikemea vikali vyama vya msingi vyenye migogoro na kuvitaka kumaliza to fauti zao.

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa Muungano huo wamesema kuwa watatoa ushirikiano wa dhati kwa uongozi uliochaguliwa ili kufikia malengo waliojiwekea katika kuwasaidia wakulima wa zao la Tumbaku Nchini.

Muungano wa Vyama vya wakulima wa Tumbaku Tanzania unaundwa na Vyama vya KACU LTD KAHAMA,WETCU LTD TABORA,CETCU LTD MANYONI,ITCOJE LTD IRINGA,KTCU LTD KIGOMA,LATCU LTD MPANDA,CHUTCU LTD MBEYA NA SONAMCU LTD SONGEA.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata