DC KAHAMA APIGA MARUFUKU KUTEMBEZA DAWA ZA MITI SHAMBA MITAANI.Serikali wilayani Kahama imewapiga Marufuku waganga wa tiba asili na tiba mbadala wanaotembeza dawa zao katika maeneo mbalimbali na kuwataka wakae katika maeneo yaliyotengwa kwaajili ya kufanya biashara hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Kahama FADHIL NKURLU wakati akizungumza na Waandishi wa habari na kusema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa waganga hao watakao bainika kukaidi agizo hilo.

Mbali na hilo NKURLU amewataka wafanyabiasha mjini Kahama kuhudhuria katika uwanja wa CDT kupata elimu ya kodi inayotelwa na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) katika wiki ya Mlipa kodi iliyoanza leo.

Amesema elimu hiyo itawawezesha wafanyabiasha kupata ulewa juu ya ulipaji kodi sambamba na kupata ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yahusiyo ulipaji wa kodi.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata