BASI LAGONGANA NA HIACHE NA KUUA WATU WATANO MORO

Watu watano wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la kampuni ya New Force lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Tunduma mkoani Mbeya.
Ajali imetokea leo Machi 4,2018 eneo la Rungemba barabara ya Morogoro- Iringa.
Basi hilo limegongana na gari dogo aina ya Toyota Hiace lililokuwa likitokea Mlali wilayani Mvomero kwenda mjini Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amethibitisha ajali hiyo akisema taarifa zaidi zitatolewa baadaye
Watu walioshuhudia ajali hiyo wameeleza chanzo ni uzembe wa dereva wa Hiace aliyekuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake, hivyo alikutana na basi la New Force lililokuwa katika njia yake.
Hiace ndilo lililoharibika zaidi katika ajali hiyo.
Na Amina Juma -Mwananchi

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata