ATUMBULIWA KWA KUPINGA WARAKA WA KKKT

Kiongozi wa Ngome ya Vijana ambaye ni Mratibu wa Masuala ya Elimu wa chama cha ACT-Wazalendo, Philipo Mwakibinga amevuliwa uanachama na chama hicho kutokana kupinga tamko la Maaskofu wa KKKT ambalo chama hicho kinaunga mkono.

Chama hicho kimesema amekuwa akitoa taarifa zinazokinzana na misimamo ya chama na kutolea mfano pia wakati wa kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilin ambapo chama kimesema alitoa tamko ambalo lilikuwa kinyume na msimamo wa chama.

Mwakibinga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Tasisi ya Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka WARAMI, aliupinga waraka huo kwa madai kuwa ulikuwa wa kisiasa wenye lengo la kukososa utendaji wa serikali na kuleta hofu kwa jamii.

ACT Wazalendo kupitia kwa Katibu Uenezi wa Ngome ya Vijana, Karama Kaila kimesema kuwa kama hajaridhika na uamuzi huo anaweza kupeleka suala lake katika kamati ya maadili ya chama hicho ili liweze kushungulikiwa zaidi

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata