ATCL YASITISHA SAFARI ZA SONGEA- DAR ES SALAAM

Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) itasitisha safari kati ya Dar es Salaam na Songea kuanzia Machi 31, mwaka huu, kutokana na ubovu wa njia ya kurukia ndege katika uwanja wa Songea.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ladislaus Matindi, safari hizo zitarudishwa baada ya kukamilika kwa matengenezo makubwa ya uwanja huo yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

“Kusitishwa kwa safari za Songea kutaathiri pia safari za Mtwara kwa kipindi kifupi kutokana na sababu za kibiashara wakati ATCL ikitathmini njia mbadala ya kuhudumia kituo hiki peke yake,” imesema taarifa.

Alisema ATCL inawaomba radhi wateja wake kwa usumbufu utakaojitokeza kutokana na uamuzi huo kwani usalama wa wateja ndio kipaumbele cha kampuni hiyo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata