ASKARI ATAKAYETOA TAARIFA ZA DEREVA ANAYEMSHAWISHI KUMPA RUSHWA ATAPANDISHWA CHEO.

Jeshi la Polisi mkoani Pwani limeanzisha kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kufuatilia madereva wanaowashawishi askari kupokea rushwa pindi wanapokutwa na makosa ya usalama barabarani na kuahidi kuwa litawapandisha vyeo askari watakamata dereva hao.


Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Pwani Jonathan Shana, amewaambia waandishi wa habari kuwa huo ni mkakati mmoja wapo wa kupambana na ajali za barabarani mkoani humo.

Aidha Kamanda Shana amefafanua kuwa kikosi kazi hicho ambacho kinaundwa na makachero kimeshaanza kazi na hatua za kisheria zitachukuliwa mara moja kwa madereva watakaokutwa na makosa hayo ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

Kamanda Shana amesema mkakati huo wa kupunguza ajali pia utalenga kuwafungia leseni pia kutangaza kwenye vyombo vya habari makampuni  yote ya mabasi ambayo yatakuwa yamekithiri kwa makosa ya mwendo kasi.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata