TOHARA KWA WANAUME YAPIGWA MARUFUKU

Wakati Serikali ya Tanzania na nchi nyingine barani Afrika zikihimiza ulazima wa tohara kwa wanaume, hii ni tofauti kabisa na nchi ya Iceland ambapo limetangaza kupiga marufuku tohara kwa wanaume na kuwa taifa la kwanza barani Ulaya kufanya hivyo.


Hata hivyo mvutano wa kupitisha muswada huo bado unajadiliwa bungeni huku kukiwa na mvutano wa kidini kati ya Wayahudi na Waislamu ambao ndio wachache kwenye bunge hilo.

Kwa mujibu wa gazeti la Times Of Israel limeeleza kuwa Muswada huo unaojadiliwa na Bunge la Iceland unapendekeza kwa mtu yeyote atakayekutwa amefanyiwa tohara afungwe hadi miaka sita jela la sivyo awe na sababu maalumu za kufanyiwa tohara.

Kwa upande mwingine Wanaharakati na Wanadiplomasia duniani wamesema kuwa hatua hiyo itazua hisia kali kwa viongozi wa kidini barani Ulaya huku wakieleza kuwa Wayahudi na Waislamu ambao ni zaidi ya 2,000+ nchini Iceland watakuwa katika hali ngumu ya maisha.

Wabunge wengi wanaounga mkono muswada huo Muswada huo wanasema kuwa tohara ya wavulana wadogo inakiuka haki yao ya kibinaadamu na ni kinyume na azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya mtoto.

Ingawaje kwenye muswada huo kuna kipengele kinachoruhusu mwanaume kufanyiwa tohara kwa sababu za kidini au afya kwa masharti ya hadi afikie miaka 18, Waislamu na Wayahudi wanapinga vikali hatua hiyo kwani inakiuka tamaduni yao ya kuwafanyia tohara watoto wadogo

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata