IGP SIRRO ATUA KAHAMA,AWATAKA MAASKARI KUZINGATIA MAADILI,AZUNGUMZIA PIA HALI ILIVYO KIBITI.

MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI (IGP) SIMON SIRRO AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI MJINI KAHAMA.


KAHAMA
Mkuu wa jeshi la Polisi Tanzania (IGP) SIMON SIRRO amewataka askari kuzingatia maadili ya kazi yao katika kuwahudumia wananchi hususani katika upelelezi wa mashauri mbalimbali ya jinai ili kurahisisha upatikanaji wa haki.

Kauli hiyo ameitoa leo wilayani Kahama katika ziara yake ya kikazi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Kahama na kusema kuwa jeshi la Polisi nchini  linaendelea kutenda haki kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuharakisha  upelelezi wa mashauri yao.

Amesema kila mwananchi anawajibu wa kulinda usalama wa nchi kwa kushirikana na vyombo vya Usalama hivyo wanapaswa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili wawezekuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Mbali na hilo (IGP) amewapongeza wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa kushirikia na jeshi la Polisi katika kutokomeza mauaji ya vikongwe,ramli chonganishi na watu wenye ulemavu wa ngozi(albino).

Kuhusu swala la la mauaji yaliyokuwa yakiendelea Kibiti Kamanda Sirro amesema tangu waweke kanda maalumu ya Kipolisi katika eneo hilo sasa amani imerejea na Kibiti imekuwa sehemu yenye usalama tofauti na ilivyokuwa zamani.

MATUKIO KATIKA PICHA

ASKARI WA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA FFU KUTOKA SHINYANGA WENYE T-SHIRT NYEKUNDU WAKIWASILI KATIKA KITUO CHA POLISI MJINI KAHAMA,PEMBENI NI ASKARI WA POLISI KITUO CHA POLISI KAHAMA.
 ASKARI WA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA FFU TOKA MKOANI SHINYANGA WAKIWASILI KATIKA KITUO CHA POLISI MJINI KAHAMA.

 BAADHI YA MAAFISA WA POLISI MJINI KAHAMA WAKISUBIRI KUMPOKEA IGP SIMON SIRRO.

 MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA IGP SIMON SIRRO AKISHUKA JUKWAANI KUKAGUA GWARIDE MAALUMU LILILOANDALIWA NA JESHI LA POLISI KAHAMA.

 MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA IGP SIMON SIRRO AKISALIMIANA NA MAAFISA WA JESHI LA POLISI WILAYANI KAHAMA.

 MAAFISA WA JESHI LA POLISI KAHAMA WAKIWA TAYARI KUMPOKEA IGP SIMON SIRRO ALIPOFANYA ZIARA KATIKA KITUO CHA POLISI WILAYANI KAHAMA.

MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA IGP SIMON SIRRO WAMBELE PICHANI AKIZUNGUMZA NA ASKARI POLISI WILAYANI KAHAMA HAWAPO PICHANI ALIPOTEMBELEA KATIKA KITUO CHA POLISI KAHAMA
 MAAFISA WA JESHI LA POLISI WILAYANI KAHAMA WAKIMSIKILIZA MKUU WA JESHI LA POLISI IGP SIMON SIRRO HAYUPO PICHANI.

 MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO AKIZUNGUMZA NA MAAFISA WA JESHI LA POLISI ALIPOTEMBELEA KATIKA KITUO CHA POLISI WILANI KAHAMA.
MAAFISA WA POLISI WILAYANI KAHAMA WAKIMSIKILIZA IGP SIMON SIRRO HAYUPO PICHANI.
MAAFISA WA POLISI WILAYANI KAHAMA WAKIWA IMARA KUMSIKILIZA IGP SIMON SIRRO
IGP SIMON SIRRO PICHANI AKIKAGUA KIKOSI CHA POLISI CHA BAADHI YA ASKARI WILAYANI KAHAMA.

MAAFISA WA POLISI KUTOKA KITUO CHA POLISI KAHAMA WAKIWA TAYARI KUMPOKEA IGP SIMON SIRRO.

BAADHI YA WANANCHI WA WILAYA YA KAHAMA WAKIWA WAMELIZUNGUKA GARI LILILOMBEBA IGP SIRRO WAKISUBIRI WAMUONE.

BAADHI YA WANANCHI WA WILAYA YA KAHAMA WAKIWA NJE YA KITUO CHA MABASI WAKISUBIRI KUMUONA IGP SIMON SIRRO.

ASKARI WA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA FFU KUTOKA MKOANI SHINYANGA WAKIIMARISHA ULINZI KATIKA KITUO CHA POLISI WILAYANI KAHAMA.

MKUU WA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO AKITOKA KATIKA KITUO CHA POLISI KAHAMA KUELEKEA KATIKA BWALO LA POLISI KUFANYA MAZUNGUMZO NA ASKARI WA JESHI LA POLISI KAHAMA.

MKUU WA JESHI LA POLISI IGP SIMON SIRRO AKITOKA KITUO CHA POLISI KAHAMA.


OCD WA WILAYA YA KAHAMA KUSHOTO AKIZUNGUMZA NA MAAFISA WA POLISI KATIKA KITUO CHA POLISI KAHAM


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata