UGUMU WA USAFIRI WAKWAMISHA WANAFUNZI UBUNGO

Wanafunzi wanaosoma katika shule za mikoa mbalimbali wamekwama katika kituo cha Mabasi cha Ubungo kutokana na matatizo ya usafiri.

Hata hivyo, Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra)ilisema imeshatoa vibali kwa ajili ya kuwasafirisha wanafunzi hao.

Wanafunzi hao tangu Desemba 2017 walikuwa likizo jijini Dar es Salaam na mikoa ya jirani baada ya shule kufungwa na leo walitakiwa kurudi shule.

Shule zinatarajia kufungua kesho Jumatatu Januari 8, 2017 na wanafunzi walionekana katika kituo cha mabasi cha Ubungo

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata