TAKWIMU: KILA BAADA YA SAA MOJA MWANAFUNZI MMOJA HUJIUATakwimu iliyotolewa na serikali ya India inaweza kukushtua ni baada ya kuonyesha kwamba, ndani ya kila saa moja mwanafunzi mmoja hujiua nchini humo.

Gazeti la Times of India limeandika kuwa, idadi ya vijana wanaojiua imezidi kuongezeka kiasi cha kuwafanya viongozi wa serikali ya nchi hiyo kuanza kuzitahadharisha familia.

Kwa mujibu wa takwimu za mwisho zilizotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya India kuhusiana na suala hilo, sababu ya vijana wengi kujiua ni utumiaji wa dawa ya kulevya, matatizo ya kisaikolojia, kugombana na watu wakubwa,  pamoja na matatizo yanayohusiana na masomo.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa, idadi ya wanafunzi waliojiua mwaka 2016 pekee ilikaribia 9500 ambapo inaonyesha kwamba, karibu kila saa moja, hujiua mwanafunzi mmoja. Ripoti hiyo pia imeyataja majimbo ya Maharashtra na Bengal kuwa yanayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiua.

Hii ni katika hali ambayo India pia inaongoza kwa kuwa na kiwango cha juu cha vijana wanaojiua duniani. Wataalamu wa mambo wanaamini kwamba kabla ya serikali kutatua tatizo la kisaikolojia kwa vijana, inatakiwa kwanza kushughulikia hali ya uchumi na kutatua matatizo ya kijamii nchini humo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata