ROMA YAMKUTA TENA,SERIKALI YAMTAKA AREKEBISHE WIMBO WAKE WA KIBAMIA.

Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo imemtaka msanii Roma kufanya maerekebisho kwenye wimbo wake wa kibamia, ambao umeonekana kukiuka maadili.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Habari Juliana Shonza alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, na kusema kuwa wimbo huo umekiuka maadili ya Mtanzania, kwa kuwa na maneno ambayo hayafai na kumtaka aurekebishe mara moja.

Pia Naibu Waziri wa wizara inayohusika na masuala ya sanaa, amevitaka vyombo vya habari kutopiga wimbo huo, mpaka pale utakapofanyiwa marekebisho.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata