AFARIKI BAADA YA KUTOA SADAKA KANISANI SUMBAWANGA

WAUMINI wa Kigango cha Muze, Parokia ya Zimba Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga waliofurika kanisani kwa ibada ya misa ya Jumapili walipatwa na taharuki kubwa huku ibada ikisimama kwa muda baada ya mwanakwaya kupoteza fahamu muda mfupi baada kutoa sadaka.

Mwanakwaya huyo akiwa na ujauzito wa miezi mitano aitwaye Flora Nandi (25) akiwa mwanakwaya wa Kwaya ya Mtakatifu Cecilia alifariki dunia akiwa anakimbizwa kupatiwa huduma katika zahanati iliyopo katika kijiji cha Muze katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga.

Mkasa unaofanana na huu ulitokea miezi sita iliyopita pale mkazi wa Mtaa wa Makanyagio katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Beatrice Kangu (48) alifikwa na umauti muda mfupi baada ya kutoa sadaka katika ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kigango cha Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda kilichopo katika Mtaa wa Makanyagio B.

IMEANDIKWA NA PETI SIYAME-habarileo SUMBAWANGA

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata