WAKAZI WA MASWA WATAKIWA KUTENGA MUDA WA KILIMO NA MUDA WA KUJIANDIKISHA KUPATA VITAMBULISHO VYA TAIFA.WAKAZI  wa Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu wametakiwa kutenga muda wa kilimo na muda wa kwenda kujiandikisha ili kupata Vitambulisho vya Taifa ambavyo vitawasaidia  kupata huduma muhimu.

Akizungumzia zoezi hilo, jana Afisa Msajili wa Nida Maswa, Martha Rexson amesema kuwa changamoto kubwa wanayokabiliana nayo kwa sasa wakati zoezi hilo linaendele ni wananchi kukwenda mashambani na kuacha kujiandikisha.

“Kwa kweli kunachangamoto kubwa.Unajua huu ni msimu wa kilimo wananchi wengi wanakwenda mashambani na kupuuzia zoezi hili. Naomba wawe wanatenga muda wa shamba na muda wa kujiandikisha,”alisema Rexson.

Aidha Rexson alibanisha kuwa tatizo la kukatika kwa umeme kila wakati nalo linawasumbua kwenye utekelezaji wa majukumu yao japo wanajitahidi kutumia njia mbalimbali kuhakikisha wananchi wengi wanasajiliwa.

“Mpaka sasa tayari tumeandikisha watu katika Kata 9 kati ya 36, Vijiji 38. Ila kukatika katika kwa umeme ni tatizo japo tunajitahidi kuhakikisha tunafanya kazi vizuri na kusajili watu wengi zaidi.”

Wakizungumzia zoezi hilo kwa nyakati tofauti wakazi wa Wilaya ya Maswa waliipongeza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NID), kwa kuwafikia na kuwasajili ilikupata vitambulisho hivyo.

“Tunapongeza Nida kwa kutufikia. Vitambulisho vya taifa ni muhimu kwetu vitatusaidia kupata mikopo na huduma nyingine muhimu,”alisema Masanja Mabula.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata