WAZAZI MKOA WA SHINYANGA WALAUMIWA KUTOTIMIZA WAJIBU WAO KATIKA MALEZI BORA YA WATOTO.Kitendo cha baadhi ya Wazazi na walezi kutotimiza Wajibu wao  katika Malezi bora kwa Watoto Mkoani Shinyanga kimetajwa kuwasababisha baadhi ya watoto kujiingiza katika makundi hatarishi ikiwemo uasherati na matumizi ya dawa za kulevya.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mratibu wa Mradi wa NITUNZE unaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la ICS kwa ufadhili wa shirika la kimataifa la Dreams International Challenges (IC) SABRINA MAJIKATA, Mjini Kahama kwenye halfa ya uzinduzi wa mradi huo.

MAJIKATA amesema kitendo hicho kimesababisha  idadi kubwa ya watoto kuanza kujitegemea wakiwa na umri mdogo jambo ambalo ni hatari katika makuzi yao.

MAJIKATA,  amesema kama wazazi na walezi  watatambua umuhimu wa malezi  bora kwa watoto ni wazi kwamba matukio ya unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo vipigo na ubakaji hayatatokea katika jamii.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama ABEL SHIJA ametoa ushauri kwa shirika la ICS kutojikita kutoa elimu kwa watoto wakike pekee na badala yake wawashirikishe watoto  wa jinsi ya kiume wanaoishi katika mazingira magumu.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata