WANAWAKE KIGOMA WALIA WAUME ZAO KUKIMBILIA KAMBI ZA WAKIMBIZI KUOA WANAWAKE WAGENI.

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
WANAWAKE Wa  Kijiji cha Kaziramihunda na Juhudi kata ya Kasanda Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma,Wamelalamikia kutelekezwa na Waume zao ambao wanatelekeza familia na kwenda kuoa wakimbizi kutoka Nchi ya Burundi na kuishi nao katika kambi ya Mtendeli Wilayani humo.

Akizungumza  katika Mkutano wa kijiji uliofanyika katika Kijiji cha Juhudi kata ya kasanda Mwenyekiti wa Wanawake hao, Tabu Kiuliko alisema Wanaume wengi katika vijiji hivyo vilivyopo karibu na kambi ya wakimbizi wengi wao wamekuwa wakitelekeza familia zao na kwenda kambini kuoa Wakimbizi jambo ambalo limekuwa Kero kwa Wamama hao na kumuomba Mkuu wa Wilaya hiyo kuwasaidia kuwarejesha.

Alisema baadhi ya Wanawake wameachwa na Watoto  zaidi ya nane na Nyumba zao zimeezuliwa na Mvua ya upepo ilionyesha mwishoni mwa Wiki hii ,Wanashindwa wafanye nini waweze kuwalea watoto wao, mpaka sasa ambapo ni msimu wa Kilimo Wanaume hao bado wapo kambini wanaishi na wakimbizi wakikwepa majukumu yao.
" Tukuombe Mkuu wa Wilaya utusaidie uende kambini uwafukuze hawa watanzania wote walioenda kuoa warundi tunaadhilika sana tumeachwa na watoto wetu hatujui tufanyaje, maisha magumu na Wanawake wengi hawana sehemu ya kwenda kulalamikia. Tukuombe utusaidie sana warudi tuweze kushirikiana nao katika shughuli za maendeleo na za kulee watoto wetu  hatuwezi peke yetu"alisema Mwenyekiti wa wamama hao.

Kwa upande wake Afisa mtendaji wa Kata ya Kasanda ,Motoni Borutu alisema suala la Wanaume wengi kukimbilia kambini hatulifurahii kabisa tumekuwa tukipokea malalamiko mengi kutoka kwa hawa Wanawake wa kijiji cha Kaziramihunda na juhudi kuwa waume zao wamekuwa  wakiingia kambini na kuoa warundi jambo ambalo halipendezi, na suala la kuoa mkimbizi linautaratibu wake.

Alisema mpaka sasa wiki mbili zilizopita kuna mwanaume mmoja aliuwawa na Wakimbizi  akiwa anatoka na Mwanamke wa Kirundi kambini hapo suala ambalo lina madhara makubwa kwani baadhi ya Wakimbizi wanachukia suala hilo na kuwafanyia unyamaa huo, na Uliwekwa utaratibu wa Wakimbizi kuingia kijijini na Wananchi kuingia kambini hairuhusiwi.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala aliwataka Wananchi hao walioingia kambini kuishi na kuoa warudi na kutelekeza familia zao kuondoka mara moja kambini humo na wale waliowaoa warundi kuachana nao .Baada ya Wiki moja ataingia kambini kuwasaka Wananchi wote walioingia kambini na kutelekeza familia zao; na kuahidi kuwashughulikia hukohuko kwa kiwa hairuhusiwi Mwananchi yeyote asiye kuingia na kuishi kambini humo.

Mkuu huyo alieleza kuwa kuna utaratibu wa Watanzania kuoa au kuolewa na Wakimbizi hairuhusiwi mtanzania kuingia kambini, alisema na kwa Wakimbizi waliohusika na mauaji ya Mwananchi huyo watatafutwa wote wakamatwe hawaweze kuwapokea wakimbizi na kuwahifadhi halafu wao wawauwe Wananchi wetu jambo hilo halikubaliki kabisa.

"Niwaombe mrudi kwenye familia zenu kukimbia matatizo sio njia ya kupunguza matatizo bali kuongeza matatizo, mzirudie familia zenu. Na wakina mama ambao waumezenu wametolokea kwa Wakimbizi njooni ofisini au ninendeni Usawi wa Jamii kueleza matatizo yenu wasipo chukua hatua nitachukua hatua mimi. Kuanzia leo nakuagiza wewe mkuu wa kambi msaidizi anzeni msako wa Watanzania wote waliohamia kambini humo na  tutawashughulikia". Alisema. "Pia nina wasiwasi hawa ndio wanao iba mashambani. Nawasihi warudi kwenye familia zao kabla ya shari", alisema Kanali Ndagala.

Hata hivyo Afisa uhamiaji Wa Wilaya hiyo , Christopher Mlemeta alisema kuingia kambini na kuoa mkimbizi hairuhusiwi kisheria, utaratibu uliopo mwanamke akitaka kuolewa na mkimbizi ni lazima aende kuishi Burundi na mwanaume Akitaka kuoa mrundi ni lazima afuate utaratibu apatiwe vibali hii ikiwa ni pamoja na kuwatumikisha Warundi mashambani bila kibali ni kosa kisheria.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata