WANANCHI WATAKIWA KUWAFICHUA WAHAMIAJI HARAMU ILI WASISHIRIKI ZOEZI LA VITAMBULISHO VYA TAIFA


Serikali mkoani Shinyanga imewataka wananchi kuwafichua wahamiaji haramu katika maeneo yao ili wasiweze kuandikishwa kwenye zoeli la vitambulisho vya taifa linaloendelea katika baadhi ya maeneo mkoani humo.


Akizungumza na wananchi wa Kata ya Nyamilagano halmashauri ya Ushetu, Mkuu mkoa wa Shinyanga, ZAINAB TELACK amesema zoezi la kuandikisha vitambulisho vya taifa limeshaanza mkoani humo na linamhusu kila Mtanzania mwenye umri wa miaka zaidi ya 18.


Amesema katika zoezi hilo, Wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa serikali ili wahamiaji haramu wasiandikishwe katika zoezi hilo na kwamba viongozi wa Vijiji na Mitaa wanalojukumu la kujiridhisha na uraia wa kila anayefika kuandikishwa.


TELACK pia amewataka wananchi wenye sifa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo pindi litakapoanza katika maeneo yao na kwamba seriakli imekusudia kutoa vitambulisho vya taifa kwa kila Mtanzania anayekidhi.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata